Baadhi ya Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakiandamana kwa amani ikiwa ni hatua ya kuonyesha hisia zao za kupinga vikali mauaji yanayofanywa na Jeshi la Polisi kwa Raia hapa nchini hususani katika rapsha mbalimbali zikiwemo za mikutano ya kisiasa ambapo hivi karibuni Mwandishi wa Chanel Ten Mkoani Iringa alipoteza maisha baada ya kushambuliwa na Polisi na kuuawa pale pale akiwa kazini (akikusanya picha za habari). 
Katibu Mkuu wa Jukwaa la Wahariri Ndg. Devil Meena akitoa tamko kwa niaba ya waandishi wa habari,baada ya maandamano eneo la viwanja vya jangwani jijini Dar.
0 comments:
Post a Comment