Sep 10, 2012

MAKAMU WA RAIS DKT.GHALIB BILALI AFUNGUA MKUTANO WA SABA WA WAKUU WA SHULE AFRIKA

 Makamu wa Rais Dkt. Ghalib Bilal akihutubia na kufungua mkutano wa saba wa wakuu wa shule Afrika (African Confederation of Principals) leo katika Ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar Es Salaam.

Naibu waziri wa Elimu na Mafunzo yaUfundi Mhe.Philipo Mulugo(Mb),akihutubia katika mkutano huo

 Pichani Makamu wa Rais Dkt. Ghalib Bilali akipewa maelezo ya kibiashara kutoka kwa Bi.Shana William kutoka S.Scientific Centre (Wuzaji wa vifaa vya Maabara kwa Shule za Sekondari hapa nchini) wakati Dkt. Bilali alipotembelea banda hilo.


 Dkt. Bilali akitazama moja ya kitabu kutoka banda la Radar Education Limited ambapo afisa biashara wa kampuni hiyo,Bw.Nabil Karatela (wa kwanza kutoka kulia katika picha) akimpa dondoo kadhaa kuhusiana na bidhaa bora wanazotoa hapa nchini
  Pichani Makamu wa Rais Dkt. Ghalib Bilali akipata maelezo kutoka kwa Kababa L. Loi(afisa masoko) wa JR Institute Of Information Technology (JRIIT) ya Arusha alipotembelea banda hilo wakati wa mkutano huu wa kimataifa wa wakuu wa shule kutoka zaidi ya nchi saba za Afrika.

 Katika picha Dkt. Bilali akisalimiana na kuona bidhaa mbalimbali kutoka kwa kina mama Wajasiliamali (Tuinuane Group) kutoka Morogora

 Dkt. Bilali akifunua (peruse) kitabu katika banda la Ujuzi Books LTD. Mbele ni Bi.Moreen Kuhenga na Bw. Yona F.Sanga(afisa mauzo) wakitabasamu.

Picha juu na chini  Dkt. Bilali aktoa ushauri mzuri wa kibiashara kwa wawakirishi hawa wa kampuni ya Ujuzi Books Ltd.

  Dkt. Bilali akisaini daftari  la wageni wakati alipotembelea banda la kampuni ya kuuza  vitabu ya MAGE GENERAL ENTERPRISES huku Bi.Jane Masatu(afisa masoko) akionesha akionesha tabasamu.

 Picha juu na chini  Dkt. Bilali alipata fursa ya kupiga picha za kumbukumbu pamoja na washiriki wa mkutano huo kutoka nchi mbalimbali.

Tunafurahi kukutana hapa na kubadilishana ujuzi wa kiutendaji na kujifunza mengi kutoka kwa            kila mmoja wetu.........
Tunafurahi kukutana hapa na kubadilishana ujuzi wa kiutendaji na kujifunza mengi kutoka kwa kila mmoja wetu.........

 Wakuu wa shule mbalimbali wakiwa katika picha ya furaha na Mhe.Kassimu Majaliwa(Mb) ambaye ni Naibu Waziri TAMISEMI.

 Kazi na Dawa........! Hapa wakuu wa shule kadhaa kama wanavyoonekana katika picha wakidodosa matirio katika moja ya banda la vitabu wakati wa mapumziko mafupi ya mkutano

 Wakuu hawa katika furaha ya kushiriki mkutano huu muhimu kwao kujifunza ujuzi zaidi kutoka kwa wadau wenzao.
Kushoto ni Mwl.F. Bilal, Mwl.P.Zachariah, Mwl. M.N Mondeya,Mwl.B. Samidai ,Mwl.J. Isarara na  Mwl. N.Gidore wote kutoka Wilaya ya Ngorongoro Arusha Tanzania.

0 comments: