Sep 4, 2012

SEVENTH-DAY ADVENTIST CHURCH KUFANYA KONGAMANO LA MAISHA BORA KATIKA UKUMBI WA WATER FRONT DAR


Kanisa la Waadventista wa Sabato limetangaza kuwa linaandaa kongamano la maisha bora kwa Watanzania linalotarajia kufanyika katika ukumbi wa Water Front Sept, 17 hadi 28 ambapo Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Kikwete.
Watoa mada waliobobea wanatarajia kuwa ni pamoja na Mhe. Prof. Wangwe, (Mawaziri) Mhe.Steven Wasira, Mhe.Dr. Hussein A. Mwinyi na Mhe.Dr Mary Nagu. 
Maada mbalimbali zitajadiliwa zikiwemo Ukimwi, Maadili kwa Jamii, Uhuru wa Dini, Ujasiriamali, Mazingira, Athari za imani za uchawi, na namna ya kudumisha amani katika nchi yetu.
Imetolewa na Mchungaji Mussa D. Mika.(wa katikati katika picha hapo juu) 0786 733 660

0 comments: