Sep 12, 2012

KAMATA KAMATA DALADALA MBOVU YAENDELEA MWENGE BUS STAND

Kamata kamata ya daladala zenye ubovu uliokithiri inaendelea katika kituo cha daladala mwenge jijini Dar.
 Katika picha anaonekana dereva wa daladala iliyopo pichania akisaini kitabu cha malipo ya faini baada ya kuandikiwa makosa ya gari lake ndani ya kituo cha daladala mwenge
 Hapa askari wa kikosi cha usalama barabarani (traffic) akimwandikia kosa dereva ambaye gari lake lilibainika kuwa katika route bila honi wala indicator siku hiyo. Katikati ni utingo wa gari hilo(konda).
 Afande Insp. Nestory Ndenje akisaini kitabu cha malipo ya faini huku dereva wa gari lililobanika na kosa akiangalia kwa umakini na kusubiri kusaini pia

Operesheni hii ni kukamata magari yote yanayofanya makosa mbalimbali yakiewmo:
kushusha pasipokituo,kukatisha ruti, sare chakavu/kuendesha daladala bila kuvaa sare, leseni, kupakia pasiporuhusiwa, kutanua pasiporuhusiwa, nk

0 comments: