Sep 7, 2012

MIILI YA ASKARI JWTZ WALIOKUFA NCHINI SUDANI YAAGWA KATIKA KAMBI YA LUGALO ,DAR LEO

 Askari wa Jwtz wakiwa wamebeba moja ya jeneza la mwili wa askari watatu  wa jeshi hilo waliofariki kwa ajali ya maji  wakivuka mto Lamada, nchini Sudani walikokwenda kulinda amani chini ya jeshi la umoja wa Mataifa muda mfupi kabla ya kuagwa kwa mili hiyo Lugalo jijini Dar es Salaam leo.

 Katibu mkuu wizara ya ulinzi  akitoa  heshima za mwisho kwa miili ya marehemu

 Mkuu wa Majeshi nchini, Devis Mwamunyange akitoa  heshima za mwisho kwa miili ya marehemu

 Mkuuwa Majeshi nchini Devis Mwamunyange   akimfariji mke wa moja ya askari waliofariki Bi. Fatuma Chunguile

 Askari wa JWTZ wakingiza miili ya marehemu katika gari tayari kwa safari ya kuelekea mikoani kwa ajili ya Mazishi


Mkuuwa Majeshi nchini Devis Mwamunyange  akiongea nawaandishi wa habari 

0 comments: