Sep 7, 2012

PICHA NA HABARI MKUTANO MKUU WA MWAKA BODI YA WAANDISI (ERB) 06-07/ 2012, MLIMANI CITY DAR



Mgeni Rasmi Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi akiwasili ukumbini. Kushoto kwake ni Msajili wa Bodi Eng.Mlote

Sehemu ya baadhi ya viongozi waliohudhulia mkutano huo. wa kwanza kutoka kulia ni Mh.Naibu Katibu Mkuu Ujenzi, wa pili ni Mhe. Katibu Mkuu (Mgeni Rasmi kwa niaba ya Mhe. Waziri), wa tatu kushoto ni Prof. Lema na wa mwisho kutoka kushoto ni Msajili wa Bodi (ERB), Eng. Mlote. 
Prof. Lema ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Waandisi nchini (ERB) akisoma hotuba yake kwa washiriki wa mkutano huo. Kushoto kwake anaonekana Balozi Juma MwapachUu akifuatilia jambo fulani katika moja ya makabrasha yaliyoandaliwa mahsusi kwa washiriki.
Mgeni Rasmi akihutubia  washiriki wa mkutano huo.

Baadhi ya washiriki akina mama wakifuatilia kwa umakini hotuba ya Mgeni Rasmi


 Washiriki wakipiga makofi kushukuru kwa hotuba nzuri ya Mgeni Rasmi

 Msajili wa Bodi Eng. Mlote akitoa  hotuba yake kwa washiriki wa mkutano huo.

 Mgeni Rasmi akapata fursa ya kukabidhi laptop,vyeti na fedha taslimu laki tatu, kama zawadi zilizotolewa  na Bodi kwa wanafunzi wa vyuo vikuu waliofanya vizuri katika masomo yao ya  sayansi ya uinjinia.

  Pichani Prof. Lema (kushoto) akimkabidhi zawadi iliyotolewa na Bodi kwa Mgeni Rasmi

 Washiriki katika picha ya pamoja na Mgeni Rasmi.

 Kushoto katika picha ni Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Eng. Simbakalia akiteta jambo na washiriki wa mkutano huo nje ya ukumbi punde baada ya picha ya pamoja.
 Mgeni Rasmi akapata fursa ya kutembelea na kupewa taarifa mbalimbali kutoka kwa washiriki wa mabanda ya maonesho ya bidhaa wanazozalisha












 Baada ya kutembelea mabanda ya maonesho ya biashara Mhe. Mgeni Rasmi akazungumza na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari.

 Siku iliyofuatia(Sept.7. 2012), Mgeni Rasmi kabla ya kufunga rasmi mkutano huo alikabidhi vyeti kwa Makampuni yaliyofanya vizuri kibiashara.
 Ndg.Manish Tripathi(afisa masoko, IMPORTS INTERNATIONAL (T) LTD ) akipokea cheti cha pongezi.





 Sr.Elizabeth akipokea cheti kwa niaba ya St. Joseph University Tanzania.









0 comments: