Sep 12, 2012

KAMATA KAMATA DALADALA MBOVU YAENDELEA MWENGE BUS STAND

Kamata kamata ya daladala zenye ubovu uliokithiri inaendelea katika kituo cha daladala mwenge jijini Dar.
 Katika picha anaonekana dereva wa daladala iliyopo pichania akisaini kitabu cha malipo ya faini baada ya kuandikiwa makosa ya gari lake ndani ya kituo cha daladala mwenge
 Hapa askari wa kikosi cha usalama barabarani (traffic) akimwandikia kosa dereva ambaye gari lake lilibainika kuwa katika route bila honi wala indicator siku hiyo. Katikati ni utingo wa gari hilo(konda).
 Afande Insp. Nestory Ndenje akisaini kitabu cha malipo ya faini huku dereva wa gari lililobanika na kosa akiangalia kwa umakini na kusubiri kusaini pia

Operesheni hii ni kukamata magari yote yanayofanya makosa mbalimbali yakiewmo:
kushusha pasipokituo,kukatisha ruti, sare chakavu/kuendesha daladala bila kuvaa sare, leseni, kupakia pasiporuhusiwa, kutanua pasiporuhusiwa, nk

MKUTANO WA 58 WA WABUNGE WANACHAMA JUMUIYA YA MADOLA (CPA) WAFUNGULIWA RASMI LEO JIJINI COLOMBO, SRI LANKA

Mhe.Spika Anne Makinda pamoja na Mhe. Zitto Kabwe(Mb) wakijongea katika ukumbi  tayari kushiriki hafla ya ufunguzi rasmi wa mkutano huo leo.

Mhe.Spika Anne Makinda ni (wa pili kushoto) waliosimama mstari wa kwanza mbele,akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mkutano huo wa madola (ACP) . Rais Mahinda Rajapaksa(katikati kwenye zuria jekundu)anaonekana pia akiwa katika pozi la picha baada ya ufunguzi rasmi wa mkutano huo.

WAANDISHI WA HABARI TANZANIA WAANDAMANA KWA AMANAI NCHI NZIMA



Baadhi ya Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakiandamana kwa amani ikiwa ni hatua ya kuonyesha hisia zao za kupinga vikali mauaji yanayofanywa na Jeshi la Polisi kwa Raia hapa nchini hususani katika rapsha mbalimbali zikiwemo za mikutano ya kisiasa ambapo hivi karibuni Mwandishi wa Chanel Ten Mkoani Iringa alipoteza maisha baada ya kushambuliwa na Polisi na kuuawa pale pale akiwa kazini (akikusanya picha za habari). Katibu Mkuu wa Jukwaa la Wahariri Ndg. Devil Meena  akitoa tamko kwa niaba ya waandishi wa habari,baada ya maandamano eneo la viwanja vya jangwani jijini Dar.

Sep 10, 2012

MAKAMU WA RAIS DKT.GHALIB BILALI AFUNGUA MKUTANO WA SABA WA WAKUU WA SHULE AFRIKA

 Makamu wa Rais Dkt. Ghalib Bilal akihutubia na kufungua mkutano wa saba wa wakuu wa shule Afrika (African Confederation of Principals) leo katika Ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar Es Salaam.

Naibu waziri wa Elimu na Mafunzo yaUfundi Mhe.Philipo Mulugo(Mb),akihutubia katika mkutano huo

 Pichani Makamu wa Rais Dkt. Ghalib Bilali akipewa maelezo ya kibiashara kutoka kwa Bi.Shana William kutoka S.Scientific Centre (Wuzaji wa vifaa vya Maabara kwa Shule za Sekondari hapa nchini) wakati Dkt. Bilali alipotembelea banda hilo.


 Dkt. Bilali akitazama moja ya kitabu kutoka banda la Radar Education Limited ambapo afisa biashara wa kampuni hiyo,Bw.Nabil Karatela (wa kwanza kutoka kulia katika picha) akimpa dondoo kadhaa kuhusiana na bidhaa bora wanazotoa hapa nchini
  Pichani Makamu wa Rais Dkt. Ghalib Bilali akipata maelezo kutoka kwa Kababa L. Loi(afisa masoko) wa JR Institute Of Information Technology (JRIIT) ya Arusha alipotembelea banda hilo wakati wa mkutano huu wa kimataifa wa wakuu wa shule kutoka zaidi ya nchi saba za Afrika.

 Katika picha Dkt. Bilali akisalimiana na kuona bidhaa mbalimbali kutoka kwa kina mama Wajasiliamali (Tuinuane Group) kutoka Morogora

 Dkt. Bilali akifunua (peruse) kitabu katika banda la Ujuzi Books LTD. Mbele ni Bi.Moreen Kuhenga na Bw. Yona F.Sanga(afisa mauzo) wakitabasamu.

Picha juu na chini  Dkt. Bilali aktoa ushauri mzuri wa kibiashara kwa wawakirishi hawa wa kampuni ya Ujuzi Books Ltd.

  Dkt. Bilali akisaini daftari  la wageni wakati alipotembelea banda la kampuni ya kuuza  vitabu ya MAGE GENERAL ENTERPRISES huku Bi.Jane Masatu(afisa masoko) akionesha akionesha tabasamu.

 Picha juu na chini  Dkt. Bilali alipata fursa ya kupiga picha za kumbukumbu pamoja na washiriki wa mkutano huo kutoka nchi mbalimbali.

Tunafurahi kukutana hapa na kubadilishana ujuzi wa kiutendaji na kujifunza mengi kutoka kwa            kila mmoja wetu.........
Tunafurahi kukutana hapa na kubadilishana ujuzi wa kiutendaji na kujifunza mengi kutoka kwa kila mmoja wetu.........

 Wakuu wa shule mbalimbali wakiwa katika picha ya furaha na Mhe.Kassimu Majaliwa(Mb) ambaye ni Naibu Waziri TAMISEMI.

 Kazi na Dawa........! Hapa wakuu wa shule kadhaa kama wanavyoonekana katika picha wakidodosa matirio katika moja ya banda la vitabu wakati wa mapumziko mafupi ya mkutano

 Wakuu hawa katika furaha ya kushiriki mkutano huu muhimu kwao kujifunza ujuzi zaidi kutoka kwa wadau wenzao.
Kushoto ni Mwl.F. Bilal, Mwl.P.Zachariah, Mwl. M.N Mondeya,Mwl.B. Samidai ,Mwl.J. Isarara na  Mwl. N.Gidore wote kutoka Wilaya ya Ngorongoro Arusha Tanzania.

RAIS KIKWETE AFUNGUA CHUO KIKUU CHA KIMATAIFA CHA JESHI LA ULINZI HAPA NCHINI

 Rais Jakaya Kikwete akikata utepe na kuzindua rasmi Chuo cha Mafuzo ya Ulinzi hapa nchini (National
Deffence College) leo Sept. 10. 2012, Kunduchi jijini Dar Es Salaam.
Kulia kwa Rais ni Mkuu wa Majeshi ya ulinzi na usalama hapa nchini, Jenerali Davis Mwamunyange, na kushoto kwa Rais ni Mkuu wa chuo hicho Meja Jenerali Charles Makalala.

 Katika picha Rais Kikwete akitembea ndani ya jengo la chuo na kutambulishwa baadhi ya maeneo.
Nyuma anaonekana Jenerali Mwamunyange akiteta jambo na Waziri wa Ulinzi Mhe.Shamsi Vuai Nahoza